Wednesday, August 24, 2011

HUSSEIN MACHOZI ARUDI TETEMESHA RECORDS LABEL ILIYOMTOA 2007

HUSSEIN MACHOZI
Artist Hussein Machozi amerejea kwenye label ya Tetemesha Recordz iliyomtoa na kumkuza kimuziki mwaka 2007
Mwaka 2010 Hussein Machozi alizinguana na uongozi wa label hiyo iliyo chini ya Kid Bway baada ya kukiuka baadhi ya masharti ya mkataba wake yaliyopelekea uongozi kuamua kusitisha kwa muda mkataba wake ili kumpa nafasi ya kupewa nguvu msanii mwingine aliyekuwa ndio anaaza kutambuulishwa mwaka jana anayefahamika kama Sajna na baadaye C-Sir Madini

SANDU GEORGE (KID BWOY) - C.E.O TETEMESHA ENTERTAINMENT
Kwa sasa Hussein Machozi amefanya makubaliano mapya na kusaini mkataba mwingine na Tetemesha Entertainment,na amesharekodi baadhi ya nyimbo mpya zitakazotoka mwaka ujao 2012,na imeshadondoshwa remix ya ngoma Unanifaa na amewashirikisha wasanii wenzake wa Tetemesha C-sir Madini na Sajna coz Version ya mwanzo ilifanyika Akhenato Records chini ya Lil Ghetto.Remix beat imefanywa na Amba,na vilivyosalia vyote vimefanyika Tetemesha Recordz
....VICHWA VYA TETEMESHA ENTERTAINMENT....

No comments:

Post a Comment