Tuesday, March 15, 2011

AT LAST LULU KAN'GAKA KUHUSU KUPIGWA MARUFUKU CLUB

STAA anayebamiza katika kiwanda cha Filamu Bongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amewachana vikali baadhi ya viongozi wa vilabu vya usiku ambao wametoa matamshi yenye kuashiria kumpiga marufuku kuingia kwenye kumbi zao zinazotoa burudani usiku kucha kwa sababu ya kuwa na umri chini  ya miaka 18, Rockcitystuners ina full data.

Akizungumza na blog hii njia ya simu siku chache baada ya viongozi hao wa vilabu kusema kwamba, watampiga biti ‘The youngest movie star’ huyo kutia pua yake katika kumbi zao za burudani, Lulu amesema anataka amuone mtu wa kumzuia kuingia maeneo hayo.

 “Nimuone huyo wa kunizuia kuingia klabu yoyote hapa mjini, nina uzoefu wa kutosha katika kumbi za burudani na hakuna ambapo sijawahi kutia maguu yangu, labda iwe sehemu iliyojengwa leo,” alisema kwa hasira Lulu.
Kama vile haitoshi, Lulu alithubutu kusema kwamba, ameanza kuingia klabu tangu akiwa darasa la sita na hajawahi kuzuiwa popote kwa kigezo cha umri kuwa mdogo, hivyo kwake inakuwa kama hadithi kwani katika historia ya maisha yake haijatokea kukutana na kitu kama hicho.

“Nimeanza kuingia klabu tangu niko darasa la sita nd’o wanikataze leo? Sijawahi kukutana na kitu kama hicho na juzi kati tu nilikuwa ‘Billz’ ( Bilicanas). Siwezi kuzuiwa kula ‘life’ na mtu yeyote, labda rais,” aliongeza kusema Lulu huku akionesha kujiamini.

Msanii huyo ambaye alijiunga katika tasnia ya filamu mwaka 2000 akitokea Kundi la Sanaa la Kaole  lenye maskani yake jijini Dar amekuwa akionekana katika kumbi mbalimbali za  usiku (klabu) huku akiwa  ‘matingasi’ tangu akiwa mwanafunzi.

Inadaiwa kwamba, hali hiyo ndiyo iliyomfanya asihimili masomo na kujikuta akishindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.
In past few days Rockcity stuners posted  kuhusu scene ya lulu  kupigwa stop club za: Sun Cirro (Ubungo), Billz (Posta) na Mzalendo Pub (Kijitonyama).

Viongozi wa kumbi hizo walikaririwa kwa nyakati mbalimbali wakisema kwamba, msanii huyo bado mdogo kiumri na kumtaka kukazania elimu kuliko kuendekeza starehe. And this is what she had to reply

No comments:

Post a Comment