Sunday, March 13, 2011

Utata kuhusu vyombo vya muziki vilivyotolewa na mkuu wa nchi...Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa wasanii nchini, umechukua sura mpya baada ya Chama cha Tanzania Fleva Unit kujitokeza na kudai kuwa vyombo hivyo viko chini yao na hakuna msanii yeyote aliyekatazwa kujiunga na chama hicho.

Hayo yaliweka wazi na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Banana Zorro, ambaye alisema vifaa hivyo viko chini yao pamoja na mtambo wa kufyatulia CD ambavyo vimehifadhiwa sehemu maalum.

"Vifaa vipo chini ya Chama cha Tanzania Fleva Unit, na sasa tayari tumeshampata prodyuza kutoka Uingereza ambaye ni mtaalamu wa studio ya kisasa (master studio), baada ya wiki moja studio itafunguliwa," alisema Banana na kuongeza kuwa baada ya wiki moja watatoa ufafanuzi zaidi.

Banana alisema, mpaka sasa chama kina wanachama 105 na bado kinahitaji wasanii zaidi huku akisisitiza kwamba hakuna msanii aliyekatazwa kujiunga na chama hicho.

Naye Katibu wa chama hicho, Lamar Niekam alisema kuwa taratibu za kusajili chama zimeshakamilika na sasa wanasubiri kufungua studio ianze kazi.

Akasisitiza ; "THT hawahusiki kabisa katika studio hii na wala Mkurugenzi wake Ruge Mutahaba, kwani hii ni mali ya wasanii wote wa Tanzania na si mtu mmoja kama inavyozushwa."

No comments:

Post a Comment