Filamu mpya ya Love Destiny siyo salama kuiangalia ukiwa na watoto, kaka na dada, achilia mbali wazazi na wakwe, Ijumaa limeiona, kwa hiyo halitanii.
Wahusika wawili wa filamu hiyo, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ (pichani) na Hemed Suleiman ‘PHD’, wameonesha vitendo vya ngono ndani yake, hivyo kutibua tafsiri iliyokusudiwa.
The Udaku Master, Ijumaa kupitia ushuhuda wake kwenye filamu hiyo, limejionea yafuatayo;
MOSI: Moja ya vipande (scene) ambavyo Aunt amecheza, amevua nguo na kubaki mtupu kuanzia kifuani mpaka kiunoni.
Tukio hilo, linaonekana waziwazi, huku Aunt kwa kujisitiri, akijifunika matiti kwa kutumia viganja vyake.
Dhamira ya mwandishi wa filamu, mtayarishaji na muongozaji, ilikuwa ni kuonesha jinsi Aunt navyomtega kimapenzi Hemed lakini wakavuka mpaka na kukiuka maadili.
PILI: Picha halisi iliyojionesha kwenye filamu hiyo, ni wazi kwamba maungo ya Aunt hususan yale ya kuanzia kiunoni hadi kichwani, hayana u-faragha wowote mbele ya Hemed, mpiga picha, muongozaji na wengine waliokuwepo.
TATU: Katika kipande kingine, Aunt na Hemed, walijaribu kuonesha uhodari wao wa kimapenzi, kwani jitihada zao za kuonesha uhalisia, zilivuka kiwango, hivyo wakacheza X.
Ndani ya ‘muvi’ hiyo, Ijumaa limejionea matukio ya ngono ambayo kwa filamu za nje, huandikwa onyo kwamba haziruhusiwi kuoneshwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka 18.
MASHUHUDA NAO WAKEMEA
Baadhi ya watu walioiona filamu hiyo, wamesema kuwa Aunt amejidhalilisha kukubali kushiriki matukio hayo ya X.
Patricia Muddy wa Sinza, Madukani aliliambia gazeti hili juzi: “Mimi ni mpenzi wa filamu lakini kitendo alichofanya Aunt ni aibu kwetu sisi wanawake.
“Imeniuma zaidi kuona kuwa ndani ya filamu ile kuna wanaume, sasa mbona wao hawajavua? Kwa nini kila siku wanawake ndiyo tunadhalilishwa na sisi wenyewe tunakubali kudhalilishwa?”
Mdau mwingine aliyetazama filamu hiyo ni Paul Asajile aliyesema: “Niliona filamu ni nzuri, nikainunua kwa sababu waigizaji wote ni wakali.
“Sijawahi kuaibika kama siku hiyo. Tulianza kuangalia vizuri, mara tukaanza kushuhudia mambo ya ngono. Nikashika rimoti ili nipeleka mbele, kumbe betri nazo hazikuwa na nguvu.
“Nimehangaika lakini watoto waliangalia, nikaona aibu kwa sababu siku hiyo na mama mkwe wangu alikuwa anaangalia video.”
ETI HAWAKUSHTUKIA
Mtayarishaji ambaye pia ni mmoja wa waigizaji wa filamu hiyo, Salama Salmin ‘Sandra’ alizungumza kwenye kipindi cha Bongo Movie, EATV kuwa hawakujua kama vitendo vile vingewakwaza wengi.
“Hatukujua kama ingefika hapo,” alisema Sandra.
DK. CHENI NAYE
Mbali na waigizaji hao, wasanii wengine waliouza sura kwenye filamu hiyo ni Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Hashim Kambi, Hidaya Njaidi ‘Mama Mcharuko’ na Farida Sabu.

Mbali na waigizaji hao, wasanii wengine waliouza sura kwenye filamu hiyo ni Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Hashim Kambi, Hidaya Njaidi ‘Mama Mcharuko’ na Farida Sabu. Atricle from(http://www.globalpublishers.info/profiles/blogs/looh-aunt)
No comments:
Post a Comment