Sunday, August 14, 2011

MSECHU ATINGA NUSU FAINALI ZA TUSKER ALLSTARS 2011 AKICHUANA NA DAVIS NA ALPHA




Kwa mara nyingine tena Msechu ameingia Top three ya Tusker All Stars akiwa pamoja na Davis na Alpha kama ilivyokuwa kwa mwaka jana. Msechu amejihakikishia nafasi hiyo kutokana na uwezo alionao wa kulishambiulia jukwaa huku akiwachezesha mashabiki wake.
Wengi wa waliochangia kwenye ukurasa wa Facebook wa Tusker Lager wameonyeshwa kumkubali Msechu huku Alpha akionyesha upinzani wa karibu jambo linalotufanya tuongeze jitihada za kumpigia kura ili walao safari hii ashinde.
Msechu amefanikiwa kufikia nafasi hiyo na kumpiku Mtanzania mwingine Hemedy ambaye alikuwa akitamba na Swaga yake ya Mwamvuli. “Hemedy ameponzwa na over confidence “ alisema shabiki mmoja. Mdau mwingine Aleen alisema “ Am just happy for Msechu but the rest surely!!!! U mean there’s no girl…u must be kidding me!” akionyesha kutoridhishwa na kutokuwepo mdada hata mmoja kwani wengi walimfagilia Amelina.

No comments:

Post a Comment