Akizungumza na blog hii njia ya simu siku chache baada ya viongozi hao wa vilabu kusema kwamba, watampiga biti ‘The youngest movie star’ huyo kutia pua yake katika kumbi zao za burudani, Lulu amesema anataka amuone mtu wa kumzuia kuingia maeneo hayo.
“Nimuone huyo wa kunizuia kuingia klabu yoyote hapa mjini, nina uzoefu wa kutosha katika kumbi za burudani na hakuna ambapo sijawahi kutia maguu yangu, labda iwe sehemu iliyojengwa leo,” alisema kwa hasira Lulu.
“Nimeanza kuingia klabu tangu niko darasa la sita nd’o wanikataze leo? Sijawahi kukutana na kitu kama hicho na juzi kati tu nilikuwa ‘Billz’ ( Bilicanas). Siwezi kuzuiwa kula ‘life’ na mtu yeyote, labda rais,” aliongeza kusema Lulu huku akionesha kujiamini.
Msanii huyo ambaye alijiunga katika tasnia ya filamu mwaka 2000 akitokea Kundi la Sanaa la Kaole lenye maskani yake jijini Dar amekuwa akionekana katika kumbi mbalimbali za usiku (klabu) huku akiwa ‘matingasi’ tangu akiwa mwanafunzi.
Inadaiwa kwamba, hali hiyo ndiyo iliyomfanya asihimili masomo na kujikuta akishindwa kufanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana.
Viongozi wa kumbi hizo walikaririwa kwa nyakati mbalimbali wakisema kwamba, msanii huyo bado mdogo kiumri na kumtaka kukazania elimu kuliko kuendekeza starehe. And this is what she had to reply
No comments:
Post a Comment